Thursday, August 23, 2012

HUYU NDIE MSHINDI WA BIBI BOMBA

                                                          Bibi Veronica Mpangala
Bibi Veronica Mpangala awa mshindi wa bibi bomba ajinyakulia Tshs 5Million katika mashindano ya bibi bomba

Tuesday, August 14, 2012

BASATA: VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUDHIBITI KAZI CHAFU ZA WASANII

Mdau wa Sanaa na mkongwe wa muziki wa dansi nchini John Kitime (kushoto) akisistiza jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu Historia ya Muziki nchini kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idaya ya Ukuzaji Sanaa BASATA Vivian Shalua na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari Godfrey Mungereza
 Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari BASATA Godfrey Mungereza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu sekta ya muziki nchini.
 Rais wa Shindano la Urembo la Miss Utalii Gideon Chipungahelo naye hakuwa nyuma katika kuchangia juu ya tasnia ya muziki nchini.
 Mzee Kassim Mapili aliwaeleza vijana hali ya tasnia ya muziki ilivyokuwa huko nyuma na mabadiliko yaliyopo sasa.   
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limevitaka vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti kazi za Sanaa zisizo na maadili kabla ya kwenda hewani ili kuepuka mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Wito huo umetolewa mapema wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa BASATA Vivian Shalua wakati akiiahirisha programu ya Jukwaa la Sanaa inayofanyika kila wiki kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa, wakati Baraza limefikia hatua nzuri ya kudhibiti hali hiyo, wadau wakuu katika kumaliza tatizo hili ni wasanii wanaotakiwa kutunga kazi bora na zenye maadili huku vyombo vya habari vikiwa na wajibu wa kuchuja kila kazi ya Sanaa inayopokelewa kabla ya kuirusha hewani.
“Basata imeshaviandikia vyombo vya habari kuvielekeza kuwa na kamati za ndani za kudhibiti maadili kwenye kazi za sanaa kabla ya hazijaenda hewani. Hili ni muhimu sana katika kujenga maadili ya mtanzania” alisisitiza Shalua.
Awali akiwasilisha mada kuhusu Historia ya Muziki nchini na hatua zake mkongwe wa muziki wa dansi nchini John Kitime alisema kuwa, kumekuwa na changamoto mbalimbali miongoni mwa wasanii wa fani hiyo hali inayoufanya usifike mbali.
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na wasanii kutozingatia sheria ya hakimiliki na hakishiriki iliyopo, kuiga midundo ya muziki kutoka nje hali inayosababisha kutokuwepo kwa muziki wenye utambulisho wa Tanzania kama ilivyo kwa
mataifa mengine ya Afrika hususan Afrika Kusini.
“Tatizo kubwa ni wasanii wetu kuiga miziki na hata tamaduni za kigeni, hatuwezi kuandaa kazi za Sanaa kufurahisha wazungu au watu kutoka nje tu, tutapotea” alionya Kitime.
Kwa upande wake Rais wa Shindano la ulimbwende la Utalii (Miss Utalii) Gideon Chipungahelo alisema kuwa, kihistoria wanamuziki wetu ukianza na wakongwe waliopo walijikita katika kuiga miziki ya Zaire hivyo kinachofanywa na wasanii wetu wa sasa ni mwendelezo tu.
“Ni wazi kazi iliyopo sasa ni kuwafanya wasanii kujikita katika utajiri mwingi wa makabila yenye midundo mbalimbali tuliojaaliwa. Hapa ndipo tunapaswa kusisitiza” alishauri Chipungajelo.
Mzee Kassim Mapili aliwaeleza vijana hali ya tasnia ya muziki ilivyokuwa huko nyuma na mabadiliko yaliyopo sasa.

PREZZOO KULIPWA BILIONI 1.4 KWA MWAKA

Gazeti la DAILY POST limeandika kuwa mshahara atakaokuwa anapokea Prezzo ni dola 720,000 kwa mwaka akiwa balozi wa One Campaign.
Fedha hizo ni sawa na shilingi bilioni 1, milioni 137 na ushee za Tanzania!
Kwa mshahara huo Prezzo atakuwa akilipwa zaidi kuliko hata viongozi wakubwa Kenya.
Mshahara wa rais Mwai Kibaki ni shilingi za Kenya milioni 3.2 sawa na milioni 57 za Tanzania na waziri mkuu Raila Odinga akipokea milioni 2.4 za Kenya huku Uhuru Kenyatta akipokea kama milioni 1.5 kwa mwezi.
Hii ndo payslip ya Prezzo:
Mshahara kwa mwezi : $40,000 (TSH 63,200,000)
Posho ya nyumba : $5400 (TSH 8,532,000)
Posho ya usafiri : $6600 (TSH 10,428,000)
Kuburudika: $5000 (TSH 7,900,000)
Matibabu: $10,000 (TSH 15.800,000)
Vingine: Passport ya kidiplomasia na walinzi wawili.
Pamoja na hivyo bado kuna marupurupu mengine yanayoufanya mshahara wake kwa mwezi kufikia karibu 189,734,400