Friday, June 29, 2012
TAMASHA LA ZIFF LATARAJIWA KUANZA HIVI KARIBUNI
Kwenu marafiki wa tamasha la Filamu la ZIFF, Tamsha linakaribia
kuanza, July 5 litang'oa nanga, are we ready?
Mwaka huu mastaa kibao watashuka Bongo. Kutoka Marekani anakuja Mario
Van Peebles. Kama umeangalia filamu ya All Things Fall Apart ya 50
Cent utakuwa umewahi kumuona huyu jamaa, mle ndani aliigiza kama baba
wa 50 Cent.
Cabo Snoop naye atadondoka kutoka Angola, yote ni kuzifanya siku tisa
za tamasha zisimchoshe mtu yoyote, bila kwuasahau mastaa wetu Bongo
kama Diamond, Linah, Barnaba, Roma na Sultan King.
Bongo Movies wao ndio wataongoza jahazi la filamu, JB, Davina, Irene
Uwoya, Jackline Wolper, Cloud na wengine wengi wataheadline katika
tamasha.
ZIFF inawakaribisha Zanzibar
Asanteni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment