baada ya vichwa vya magazeti kadhaa ya bongo kuandika kwamba BARAZA LA SANAA TANZANIA
(BASATA) limetangaza kuufungia wimbo wa HAKUNAGA wa SUMALEE, katibu
mkuu wa Baraza hilo amezungumza katika EXCLUSIVE na millardayo.comGonche Materego amesema baraza hilo mpaka sasa hivi HALIJAUFUNGIA wimbo huo, lakinilimekua na majadiliano makubwa kuhusiana na nyimbo nyingi za wasanii wa Tanzania ambazo
tungo zake ZINAHARIBU lugha ya kiswahili ambapo HAKUNAGA ndio
uliozungumziwa sana kama MFANO kwa sababu kiswahili kilichotumika ndani
yake SIO SAHIHI.Materego amesema wimbo huo ulizungumziwa saaaaana, na hata watu wengine wa kawaida
ambao hawafanyi kazi na BASATA walisema kwamba UNAPOTOSHA KISWAHILI na
kwa vile wasanii ni walimu wakuu wa kiswahili ni rahisi sana watu wa
kawaida kutumia lugha za wasanii wakidhani kuwa ni sahihi lakini sio.“wenzetu wa baraza la kiswahili wameona kuna haja ya kukaa na kujadiliana kuhusiana na tatizo
la kiswahili kuharibiwa kwenye nyimbo za wasanii, tutakutana na wasanii
tusikie wanachokisema na wananchi pia wasiki ili tupate michango mizuri
zaidi kabla hatujakaa BASATA na BAKITA kuandaa mipango zaidi” ameamplfy
Materego.
hiyo ndio story kutoka BASATA na BAKITA! nipe maoni yako kuhusiana na unachofikiria………?! Habari na millardayo.com
No comments:
Post a Comment