Wednesday, July 25, 2012

TBL YAIKABIDHI SIMBA MILIONI 20 KWA AJILI YA MKUTANO

 
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ (wa pili kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kupokea hawala hiyo.

 
Kaburu akipokea hawala hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Sheria wa TBL, Kelvin Kilindo, wanaoshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
 Kilindo akiwashukuru wote waliofika kwenye mkutano huo.
 Kaburu  akiishukuru TBL kwa msaada wao na watu waliohudhuria mkutano huo.  KAMPUNI ya Tanzania Breweries (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro, leo imeikabidhi klabu ya Simba, hawala ya shilingi milioni 20, kwa ajili ya kufanikisha mkutano wake mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti, 5 mwaka huu. Makabidhiano hayo yamefanyika makao makuu ya TBL, Ilala, Mchikichini jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment