Friday, July 20, 2012

YATOLEWA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO



Shughuli ya kutafuta maiti kwenye ajali ya meli iliyozama nchini Zanzibar ilianza leo mapema huku watu miamoja wakiwa bado hawajapatikana baada meli iliyokuwa inaelekea kisiwani Zanziabr kuzama eneo la Chumbe.

Meli hiyo ilitoka Dar Es Salam jana mcahan kuelekea kisiwani ikiwa imebeba watu miambili tisini.

Hadi kufikia sasa maiti 31 wamepatikana huku watu zaidi ya 150 wakiokolewa.

Msemaji wa polisi nchini Zanzibar aliambia shirika la habari la AFP kuwa kwa sasa kuna hofu ya kutopatikana manusura wowote waliokuwa katika meli hiyo ya MV Skagit

"shughuli ya kuwatafuta manusura na maiti inaendelea lakini kwa sasa ni vigumu kwa kweli kupata manusura." alinukuliwa akisema msemamji huyo wa polisi.

Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Tanzania Visiwani ya tangaza siku tatu ya maombolezo.

 

No comments:

Post a Comment