Friday, June 29, 2012

KHADIJA KOPA, AT, KANGA MOKO NA OMEGA BWAYS KUWASHA MOTO REDDS MISS TANGA 2012

Khadija Kopa.
Msanii AT. Washindi wa tuzo za Kili Music Award, Khadija Kopa na AT wamethibitisha kutumbuiza katika onesho la kumsaka mrembo wa mkoa wa Tanga litakalofanyika tarehe 6 Julai 2012 katika uwanja wa Mkwakwani. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ipsha Media Productions and Promotions ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Shabani Tolle amesema maandalizi ya shindano hilo yamekamilika na kuahidi kuwa onesho hilo litakuwa ni moto wa kuotea mbali. Aidha Tolle amewataka wakazi wa Tanga na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kushuhudia onesho hilo na kufafanua kwamba wameamua kufanyia katika uwanja wa Mkwakwani ili kuwapa nafasi wakazi wote wa jiji hilo kuweza kushuhudia mrembo wao anavyopatikana. Wakati huo huo mkurugenzi huyo ameyashukuru makampuni mbalimbali yaliyojitokeza kufadhili shindano hilo na ikiwemo TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, Tanzania Distilleries Limited kupitia kinywaji chake cha Dodoma Wine, Tanga Beach Resort, Star Times Limited, Clouds Media Group, Integrated Communications Limited, Mwambao FM ya Tanga, Club La Vida Loca, Screen Masters na DJ Big Kim. Pia Tolle ametoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini shindano hilo na kusisitiza kuwa nafasi ya udhamini bado ipo wazi kwa yeyote anayetaka kuunga mkono katika shughuli hiyo muhimu. Naye Mratibu wa shindano hilo, Salum Mkambala, amesema kuwa kampuni yake imejipanga vizuri kufanikisha shindano hilo haswa katika suala zima la burudani huku wasanii Khadija Kopa na AT wakiahidi kuonesha burudani ya kukata na shoka na kuwathibitishia wakazi wa Tanga kuwa kura walizowapigia na hatimaye kuwawezesha kupata Tuzo za Kili Award hazikuwa za kubahatisha. Naye msanii Omega Bways ambaye ndie msanii mwenyeji ameahidi kutowaangusha wakazi wa Tanga na kuwataka wajitokeze kwa wingi katika shindano hilo huku wasanii maarufu wa Kanga moko wakipania kuiteka Tanga kwa shoo zao ambazo wameziboresha zaidi

No comments:

Post a Comment